Open top menu
#htmlcaption1 SEA DICAT POSIDONIUM EX GRAECE URBANITAS SED INTEGER CONVALLIS LOREM IN ODIO POSUERE RHONCUS DONEC Stay Connected
Alhamisi, 25 Mei 2017
Mwana funzi wa kidato cha nne apandishwa kizimbani kwa kosa la mauaji




Mwanafunzi wa kidato cha nne wa shule ya Sekondari Njechele wilayani Kinondoni, Salum Daudi (18) ni miongoni mwa washtakiwa watatu waliopandishwa kizimbani jana kwa kosa la kufanya uhalifu kwa kutumia bastola.

Daudi, pamoja na washtakiwa wengine; Peter Onesmo (23), Yohana Peter maarufu Kube (27) na Juma Hemed (22) walipandishwa jana katika mahakama ya Hakimu Mkazi, Kinondoni kwa kosa la kupora Sh1 milioni kwa kutumia bastola na panga katika tukio hilo.

Wakili wa Serikali, Grace Lwila akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Kelvin Mhina, alidai washtakiwa hao walitenda kosa hilo Machi 9 eneo la Madale, jijini Dar es Salaam.

Katika hati ya mashtaka, Lwila alidai kuwa vitu vingine vilivyoporwa katika tukio hilo ni pamoja na vocha, simu mbili ambazo washtakiwa hao wanazitumia.

Mahakama hiyo ilielezwa kuwa simu hizo ni mali ya Meshack Costantino.

Lwila alidai kuwa washtakiwa hao kabla ya kutenda kosa hilo walimtishia Hillary Justine na Samwel Leonard kwa silaha, wakiwa nyumbani kwao ili waweze kujipatia mali hizo jambo ambacho ni kinyume cha sheria.

Washtakiwa hao walikana kosa na upande wa Jamhuri uliomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa kwa sababu upelelezi unaendelea.

Hakimu Mhina alisema shtaka hilo halina dhamana, hivyo kesi hiyo iliahirishwa hadi Juni 6 itakapotajwa tena.
Read more
 Kafulila Afunguka Baada Ya Profesa Muhongo Kutumbuliwa



Aliyewahi kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu David Kafulila ameibuka na kutoa ya moyoni baada ya maamuzi yaliyofanywa na Rais Magufuli baada ya kupokea ripoti ya Kamati Maalum kuhusiana na uchunguzi wa makontena 272 ya makinikia yaliyokuwa  tayari kwa kusafirishwa nje ya nchi .
 
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Kafulila ameandika yafuatayo,
  1. Naipongeza Kamati kwa kazi iliyotukuka iliyojaa majaribu ya rushwa kubwa kwani kampuni nyingi madini, mafuta na gas duniani zina sifa hiyo kama alivyopata kusisitiza Profesa Joseph Stirglitz gwiji la uchumi na utandawazi duniani.
  2. Zaidi hatua aliyo chukua Rais kuhusu uharamia huu katika sekta ya madini inapaswa kuungwa mkono na kila mzalendo kwani imekuwa hoja ya upinzani na kila mzalendo kwa miaka mingi iliyoishia kubezwa na kupuuzwa.
  3. Rais asiishie kutaka uchunguzi kufanywa dhidi ya watumishi katika sekta ya madini tu, nchi hii imeoza, uchunguzi ufanywe mpaka ndani ya Idara ya Usalama na vyombo kama TAKUKURU kwani mafisadi hawa waliweka mfumo mzima mfukoni kwa kujenga mahusiano na baadhi ya wanausalama na vyombo vingine vyeti kiuchunguzi.
  4. Namshauri Rais aboreshe Idara ya Usalama kwa kuwa na kitengo cha ujasusi wa kiuchumi (Economic Intelligency) kitakachoweza kumudu kukabiliana na uharamia ktk utoroshaji utajiri wa nchi (illicits flows) kwani nchi inavuja kwa miaka mingi na mtandao wa uharamia huu uliweka sehemu kubwa ya mfumo mfukoni.
  5. Kuna haja yakutazama Katiba yetu upya ili ikibainika hata Rais kama alihusika na ufisadi afikishwe kwenye mkondo wa sheria kwani nchi nyingi za Africa zimeoza kwa ufisadi kuanzia Ofisi Kuu, huko ndio vinatoka VIMEMO kuruhusu uharamia wa namna hii. Ni Ushauri wangu kwa Rais aruhusu mchakato wa Katiba ili pamoja na mambo mengine tuangalie mfumo wa Ofisi Kuu kama moja ya chanzo cha uozo na uharamia huu.
  6. Ni vema Mheshimiwa Rais akatambua kwamba kampuni hizi za kimataifa zinaiba duniani kote ikiwemo Ulaya na Marekani, isipokuwa huku kwetu zinaiba zaidi kutokana na sera duni, sheria dhaifu, mifumo ya usimamizi dhaifu na udhaifu wa wanaopewa nafasi kwa ujumla. Kukabili tatizo hili lazima kutazama kwa mapana na kutengeneza mfumo madhubuti.
  7. Mwisho nimshauri Rais kwamba pamoja na kuchukua hatua hizi za kisheria za ndani, azifikishe kampuni hizi kwenye Mahakama za Kimataifa (Arbitration court) kama inavyo tamkwa kwenye mikataba ili kuzidai fidia kwa miaka yote ya Mikataba yao.
Mitambo na mali zao zishikiliwe mpaka kesi itapomalizika. Na hili lisisomeke kwamba nikukimbiza wawekezaji bali nikukabili uharamia wa utoroshaji rasilimali ambao hata sheria zakimataifa zinapiga vita. Hili ni muhimu sana. Umma una paswa kusimama pamoja dhidi ya uharamia huu!

Read more
Jumatatu, 22 Mei 2017
no image
Follow this link to join my WhatsApp group: https://chat.whatsapp.com/JfU69w22mhvAnUjV4hbJWc
Read more
Jumanne, 16 Mei 2017
Maajabu Jijini Mwanza: Mti Wagoma Kung'olewa......Ilikuwa Kila Ukikatwa Unalia Kwa Sauti Kupinga Kung'olewa


SeeBait
Wakazi wa Barabara ya Iloganzala  Jijini Mwanza jana walipigwa butwaa baada ya mti kutoa sauti kama binadamu ukipinga using'olewe. 

Tukio hilo limetafsiriwa kuwa la kishirikina ama mazingaombwe ikizingatiwa kwamba si jambo lenye uhalisia mti kuongea kama binadamu. 

Katika eneo la Iloganzala Jijini Mwanza kuna upanuzi wa barabara inayoelekea Uwanja wa ndege wa Mwanza. 

Shughuli ya kuung'oa mti huo aina ya mwembe  leo imeendelea ikiwa ni siku ya pili ya kukabiliana na mwembe huo na hatimaye wamefanikiwa kuung'oa huku mamia ya wananchi wakishuhudia tukio hilo la ajabu

Read more