Kaburi la miaka 3,700 la mwana wa kike wa Pharaoh linaamika kupatikana karibu na mabaki ya piramidi iliogunduliwa Misri.
Wizara ya mambo ya kale imesema kuwa kaburi hilo lililopo katika eneo la kifalme la Dahshur Kusini mwa Cairo lilikuwa na sanduku la mbao lililochongwa.
Ndani ya sanduku hilo kulikuwa na mitungi iliojaa nguo za mapambo vikiwemo viungo vya marehemu ambaye ni mwana wa kike wa mfalme Emnikamaw.
Piramidi hiyo ya mfalme ina urefu wa mita 600 kutoka kwa kaburi hilo.
Mwezi uliopita watalam wa vitu vya kale wanaochunguza mabaki ya jengo hilo walipata afueni kwa kupata picha za mabaki hayo zilizokuwa na jina la Emnikamaw.
Pia waligundua mabaki ya makaburi ya mawe.
Dahshur ni eneo ambalo mfalme Sneferu wa awamu ya nne alijenga piramidi ya kwanza yenye urefu wa futi 341 iliokuwa na upande mmoja ambao ulikuwa umelainishwa takriban miaka 4000 iliopita.
Pia alijenga piramidi ya awali iliokuwa na urefu wa mita 105 ambayo mteremko wake ulikuwa na ngazi zilizobadilishwa kutoka pembe yenye digree 54 hadi 43.
Mfalme Sneferu alirithiwa na mwanawe Khufu anayejulikana sana kwa kujenga Piramidi kubwa katika eneo la Giza ambayo ilikuwa na urefu wa mita 138 ambayo ilikuwa maajabu ya dunia wakati huo.
0 comments