Sasa ni rasmi fainali ya UEFA Champions League msimu wa 2016/2017 itazikutanisha timu za Real Madrid ya Hispania dhidi ya Juventus ya baada ya Real Madrid kufanikiwa kuitoa Atletico Madrid katika mchezo wa nusu fainali wakati Juventus wakiitoa Monaco.
Real Madrid leo imekutana na kipigo cha magoli 2-1 katika uwanja wa Vincente Calderon kutoka kwa wenyeji wao Atletico Madrid lakini wamefuzu fainali kutokana na mchezo wa kwanza kuifunga Atletico magoli 3-0 hivyo wameitoa kwa jumla ya magoli 4-2.
Mchezo wa fainali wa UEFA Champions League msimu wa 2016/2017 utachezwa katika uwanja wa Taifa wa Wales mjini Cardiff katika ya Real Madrid dhidi ya Juventus June 3 2017.
VIDEO: Alichoamua Rais wa Simba baada ya kupokwa point 3 na TFF vs Kagera
0 comments